KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, September 14, 2010

Nusura apoteze maisha kwa misifa


KIJANA mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, nusura apoteze maisha baada ya kuruka majini akitokea kwenye kivuko baada ya kutaka kuonyesha ufundi wake wa kuogelea na hatima yake kuokolewa.
Tukio hilo lilitokea majira ya alasiri juzi, baada ya kija huyo aliporuka kutoka kwenye kivuko cha MV Magogoni kilichokuwa kikielekea Kigamboni.

Kijana huyo aliwashangaza watu wengi waliuokuwa katika kivuko hicho baada ya kijana huyo kabla kivuko hicho hakijatia nanga aliruka kurukia majini.

Hivyo kutokana na tukio hilo ambalo lilionekana kuwa kivutio cha walio wengi ndani ya kivuko hicho, kijana huyo alikuwa akionyesha ufundi wa kuogelelea hatima maji hayo yalionekana kumzidi nguvu na wataalamu wa maji kwenda kumuokoa kijana huyo ambaye alionekana si mtaalamu wa kuogelea.

“Kijana huyo mara baada ya kuokolewa na wataalamu hao alionekana kuchoka na kukiri hakuwa mtaala na kukiri kuwa katika fikira zake aliona palikuwa karibu na kivuko na alikuwa anataka kupata uhakiki kama angeweza kufika mwenyewe.

Hata hivyo kijana huyo alikuwa matatani na kuambiwa na moja ya maaskari kuwa atafikishwa kituoni kutokana na tukio lake hilo

No comments:

Post a Comment