KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, September 17, 2010

Wagombea wabezana, Slaa aahidi elimu, JK apondaKATIKA mchakamchaka wa kuelekea uchaguzi mkuu na wagombea kila mmoja akimwaga sera zake mikoani, Mgombea kwa tiketi ya Chadema, Dk. Wibrold Slaa amekuwa akitoa ahadid ya kutoka elimu bure kuanzia ngazi ya awali hadi elimu ya juu.

Nae mgombea wa CCM , Jakaya Kikwete alikuwa akiwatahadharisha wapiga kura kuwa makini na ahadi hewa wanazomiminiwa na mgombea huyo kwa kuwa hana uwezo wa kutekeleza.

"Hizo ni ahadi hewa, kuweni makini, akili ni nywele kila mtu ana zake" Kikwete

Kikwete alisema ahadi anayotoa mgombea huyo ni sawa na kuwaongopea watoto wadogo, na kusema kwa upande wake aliwaaahdi wananchi kuwa elimu itapanda na shule za sekondari zitaongezeka na kweli sasa kila kata nchini ina shule ya sekondari na kila mtanzania atasoma ngazi ya sekondari" alisema

Na shule hizo si rahisi mtoto asome bure kabisa ila kuna mchango mdogo tu wa kuwezesha kukua kwa shule hizo, kama ujenzi wa nyumba za walimu, maabara na hata ununuzi wa vitabu.

Dk. Willibrod Slaa aliahidi kuwa pindi wananchi wakimchagua kuwa rais wao akiingia Ikulu, atahakikisha elimu itatolewa bure na kuzalisha walimun wengi na kupeleka walimu nje kwa ajili ya kukuza elimu zao.


Slaa hivi karibuni amekumbwa na kashifa ya kunyang'anya mke wa mtu na kumuweka katika hoteli na tayari mume wa mwanamke huyo amefika mahamani kutaka kulipwa fidia na mgombea kwa kumnyang'anya mke wake

No comments:

Post a Comment