KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, September 16, 2010

0fisa ajimiminia risasi MdomoniMWILI wa aliyekuwa Ofisa Usalama wa Taifa , aliyetambulika kwa jina la Mzee Mnyete
(32), umekutwa ukiwa kitandani chumbani kwake baada ya kujiua mwenyewe.

Mwili huo umekutwa chumbani kwake maeneo ya Makumbusho Kijitonyama Block 'A' katika nyumba za maofisa ya usalama wa Taifa baada ya ofisa huyo kujimiminia risasi mdomoni na hatima yake risasi hizo zilitokea kichwani.

Kamanda wa Polisi, Bw.Elias Kalinga amethibitisha tukio hilo, n kusema, kifo hicho kiligundulika jana baada ya afisa huyo kutoonekana kazini na alaitakwia ofisini kwa ajili ya kazi maalum na wenzake waliona ni vizuri wamfatilie nyumbani kwake na ndipo kifo hicho kilipogundulika.

Alisema, majira ya saa 3 kasorobo asubuhi jana, wenzake walifika nyumbani kwake na kukutwa mlango umefungwa lakini walipochungulia ndani waliona mwili huo upo kitandani na walipokuwa wakigonga waliona marehemu huyo hashituki ndipo walipochukua uamuzi wa kuvunja mlango na kugundua alikuwa amejiua mwenyewe .

Kwa haraka waliona ofisa huyo alijimiminia risasi zilizoonekana zimetokea kichwani, sababu ya kujiua afisahuyo bado haijafahamika na ripoti zaidi kutolewa

No comments:

Post a Comment