KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, September 16, 2010

UN yaonya hatari katika kambi

Mchunguzi maalum wa Umoja wa Mataifa amesema kambi za watu waliokimbia makazi yao, ni maeneo hatari kwa watoto waliokumbwa na vita



Watoto katika kambi Darfur


Radhika Coomarasamy, ambaye ameandaa taarifa kuhusu kambi hizo kwa baraza la haki za binaadam ya Umoja wa Mataifa, amesema hakukuwa na ulinzi wowote kwa watoto.

Bi. Coomarasamy amesema watoto hao wapo katika hatari ya kunyanyaswa kijinsia na pia kulazimishwa kujiunga na makundi ya watu wenye silaha.

Watoto wengi kama hao, kwa maelfu wanaishi kwenye kambi nchini Sudan, Chad na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo




Wakimbizi wa Rwanda


Wapo katika kambi hizo kwa sababu ya kukimbia vita na kuwa na matumaini kuwa watapata salama, lakini kwa watoto, kambi hizo mara nyingi si salama kabisa, amesema Bi. Coomarasamy.

Katika kuandaa ripoti hiyo kwa ajili ya baraza la haki za binaadam, mchunguzi huyo alitembelea kambi kadhaa, kati ya hizo zikiwa katikia eneo la Darfur la Sudan.

"Kitu cha kwanza mtu unakiona, ni kambi hizo ni maeneo hatari, yaani unakutana na watoto ambao wamenyanyaswa kijinsia wakati wakienda kutafuta kuni au kwenda kujisaidia porini, - kwa hiyo ni maeneo hatari," amesema Bi. Coomarasamy.

"Kitu cha pili, ni maeneo ya watu wasio na shughuli yoyote. Kuna hali ambapo watoto wanachukuliwa na makundi ya wanamgambo na hivyo wengi wamechukuliwa na kundi moja ama jingine."

Kwa hakika, kambi hizi hivi sasa ni eneo kubwa la makundi ya wanamgambo kutafuta askari watoto



Askari watoto DRC


Bi. Coomarasamy amesema sababu kuu ya watoto kukosa ulinzi ni kwa kuwa hakuna sare maalum kwa wakazi wa kambi hizo.

Baadhi ya kambi, zinaendeshwa na Umoja wa Mataifa, nyingine zinaendeshwa na mashirika ya misaada, na baadhi ya kambi hizo zinaendeshwa na serikali, nyingine zina shule na nyingine hazina.

Hatua ya kwanza katika kuleta usalama kwa watoto waliokimbia makazi yao, anasema Bi. Coomarasamy, ni hakikisho kwa watoto wote kuwa wanapata japo elimu ya kawaida, ili wasiweze kuchukuliwa na wanamgambo, na pia kuwapatia watoto hao ujuzi, ili waweze kuendesha maisha yao upya tena

No comments:

Post a Comment