Wasiwasi mazungumzo ya amani
Mazungumzo mapya kati ya Israel na Palestina yanaanza nchini Misri, huku kukiwa na wasiwasi kufuatia kumalizika kwa muda wa amri ya ujenzi katika Ukingo wa Magharibi.
Clinton, Netanyahu,na Abu Mazen
Abbas na Netanyahu
Katika hotuba yake siku ya Jumapili, Bw. Netanyahu, waziri mkuu wa Israel alisema baadhi ya maelfu ya nyumba mpya zilizopangwa kujengwa katika Ukingo wa Magharibi, hazitajengwa, lakini alisema, amri ya kusitisha ujenzi huenda isiendelezwe mara muda wake utakapokwisha Septemba 26.
"Hatutasitisha maisha ya wakazi," alisema.
Hata hivyo, msuluhishi mkuu wa Palestina Saeb Erakat amesema hakutakuwa na "suluhu nusu" na Israel.
"Kama Israel itaamua kuendeleana ujenzi wowote wa makazi, hii inamaanisha itakuwa imetibua mchakato wote wa amani, na Israel ndio itabeba lawama kwa hilo" amesema Saeb Erakat akizungumza na shirika la habari la AP
Clinton, Abbas na Netanyahu
Kikwazo kingine kinachowakabili wasuluhishi ni kuwa, eneo moja tu la Palestina limewakilishwa katka mazungumzo hayo, kwa sababu kundi la Hamas ambalo linadhibiti Ukanda wa Gaza, linapinga mazungumzo hayo.
Mmoja wa vigogo wa Hamas, Mahmoud Zahar, ameiambia BBC kuwa kundi hilo halitafanya jitihada zozote za kuzuia mazungumzo hayo kwa sababu "yatafikia kikomo kama mengine yaliyotangulia".
Lakini amesema hakuna Mpalestina yeyote, wakiwemo waliomo katika mazungumzo hayo, anaamini yataleta matokeo murua
No comments:
Post a Comment