KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, September 4, 2010

Uchaguzi wa urais wanukia Guinea



Wiki chache tu kabla ya kufanyika kwa duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Guinea, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, ametoa pendekezo kwa utawala wa kijeshi nchini humo kuipa wizara ya mambo ya ndani madaraka zaidi ili kusimamia uchaguzi huo.

Waziri Mkuu Jean-Marie Dore amependekeza kuwa kiongozi wa kijeshi nchini humo Generali Conate, aagize wizara hiyo kusimamia zoezi hilo kwa ushirikiano na tume huru ya uchaguzi.

Lakini mmoja wa wawaniaji wa kiti hicho cha urais, Cellou Dalein Dellou, amesema pendekezo hilo litamsaidia mpinzani wake Alpha Conde.

Waandishi wa Habari wanasema duru hiyo ya pili ya uchaguzi wa urais ambao utahusisha watu wawili kutoka kabila tofauti, huenda ukazua hali ya wasi wasi.



Vifo vyaongezeka nchini Guinea




Takriban watu 87 wameuawa baada ya majeshi ya Guinea kuwafyatulia risasi kundi kubwa la waandamanaji kwenye mji mkuu wa Conakry.

Kutokana na chanzo kimoja cha polisi, idadi ya watu 58 walioripotiwa kufariki dunia hapo awali imeongezeka kufikia 30.

Inakadiriwa watu 50,000 waliandamana kumpinga Kapteni Moussa Dadis Camara aliyechukua madaraka nchini humo mwaka jana.

Kapteni Camara alitwaa madaraka baada ya kufanya mapinduzi yasiyohusisha umwagikaji damu.

Maandamano hayo yaliibuka baada ya Rais Camara kubadilisha msimamo wake wa kutogombea urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Januari.

No comments:

Post a Comment