KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, September 4, 2010

Pingamizi la Chadema baada ya siku 5


MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, amesema atatolea uamuzi pingamizi lililotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Septemba 6, mwaka huu, dhidi ya Rais Jakaya Kikwete
Tendwa alisema hayo juzi mara baada yak upokea pingamizi hilo na kwuaambia waawndishi wa habari kuwa atatolea uamuzi dhidi ya pingamizi hilo baada ya siku tano.

Tendwa alisema anatoa uamuzi huo baada ya kupitia vizuri pingamizi hilo na kuzifanyia kazi hoja zilizowasilishwa na CHADEMA kwa mujibu wa sheria hiyo ya gharama za uchaguzi nchini.

Alisema anatarajia kutoa maamuzi ya haki kwa pande zote na atatoa nakala mbili ya maamuzi hayo moja kwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) pamoja na kwa makatibu wakuu wa vyama husika.

Juzi Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, aliwasilisha malalamiko hayo katika ofisi za msajili kumpa pingamizi mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amekiuka kifungu cha sheria no 21 (1) (a) hadi (e) cha sheria hiyo Na. 6 ya 2010 katika kipindi hiki cha kampeni kwa kutoa ahadi katika uzinduzi wa kampeni zake..

Pingamizi hilo lilikuwa na malalamiko makuu matatu, likiwamo la mgombea huyo kuongeza na kupandisha kima cha chini cha mishahara ya wafanyakazi kutoka 135,000 hadi kufikia shilingi 235,000, ambapo Bunge la Jamhuri ya Muungano halikudhihirisha hilo..

Mengine ni kuahidi kukipa Chama cha Ushirika cha Nyanza, shilingi billion tano ili kilipe madeni ambayo kinadaiwa na kuahidi kuwa serikali itachukua madeni yote ya vyama vya ushirika na kuwaahidi watu wa Mkoa huo kuwanunulia meli mpya kubwa na ya kisasa zaidi.

No comments:

Post a Comment