KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 20, 2010

Uchaguzi wa Urais wahairishwa-Guinea


Machafuko ya kisiasa nchini Guinea

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Magharibi mwa Afrika, amewasili nchini Guinea kwa awamu mpya ya mazungumzo, kuhusu duru ya pili ya uchaguzi wa urais ambao umehairishwa.

Uchaguzi huo ambao uliopangiwa kufanyika leo umehairishwa na tume ya uchaguzi nchini humo haijatangaza tarehe mpya ya uchaguzi huo wa urais.

Wakati wa ziara hiyo, mjumbe huyo Saif Djinnit, anatarajiwa kufanya mazungumzo na maafisa wa tume ya uchaguzi, kaimu rais wa taifa hilo Sekouba Konate na wawaniaji wawili wa urais, Cellou Dalein Diallo na Aplha Conde.

Duru hiyo ya pili iliahirishwa baada ya mtu mmoja kuuawa na wengine 50 Kujeruhiwa kwenye makabiliano makali kati ya wafuasi wa wawaniaji hao wa urais wiki moja iliyopita

No comments:

Post a Comment