KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 20, 2010

Acheni kumiliki silaha za maangamizi-Mubarak



Acheni kumiliki silaha za maangamizi-Mubarak

Rais Mubarak na Benjamin Netanyahu
Rais wa Misri Hosni Mubarak, ametoa wito wa moja kwa moja kwa serikali ya Israel huku akiwahimiza viongozi wake kutia saini azimio linalopiga marufuku kumiliki na kusambazwa na silaha za nuklia.

Katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni nchini Israel, Rais Mubarak amesema anataka kuona eneo la Mashariki ya Kati kuwa eneo lisilokuwa na silaha za maangamizi.

Rais huyo amesema hajali ikiwa silaha hizo zinamilikiwa na Iran au Israel.

Serikali ya Israel inaaminika kumiliki silaha za nuklia lakini madai hayo hayajathibitishwa.

Iran imepuuzilia mbali madai kuwa mradi wake wa nuklia unanuiwa kuunda silaha za maangamizi.

Mataifa ya Kiarabu yamekuwa yakitaka mataifa yote ya Mashariki ya Kati kutomiliki silaha zozote za maangamizi.

Suala hili linatarajiwa kijadiliwa katika mkutano wa kila mwaka wa shirika la umoja wa mataifa linalothibiti masauala ya nuklia IAEA ambao unaanza hapo kesho.

No comments:

Post a Comment