KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 20, 2010

Tarehe ya uchaguzi Nigeria yahojiwa


Kampeni zimeanza Nigeria



Chama tawala cha Nigeria kimesema kufanya uchaguzi mwezi Januari, kama ilivyopangwa, itakuwa vigumu.

Msemaji wa PDP Rufai Ahmed Alkali, hata hivyo, alikataa kutoa wito rasmi wa kuchelewesha uchaguzi huo, akisema inaweza "kueleweka tofauti."

Siku ya Jumapili, maafisa wa uchaguzi wamesema walikuwa wakitazama namna ya kuuchelewesha uchaguzi ili waweze kulirekebisha daftari la kujiandikisha wapigia kura liwe lenye kuaminika.

Idadi kubwa ya viongozi waandamizi wanataka kugombea nafasi ya urais.

Mwishoni mwa juma, mshauri wa Rais kuhusu usalama Aliyu Gusau alijiuzulu ili aweze kugombea dhidi ya Rais Goodluck Jonathan ndani ya chama hicho.

Chama cha PDP (People's Democratic Party) kimeshinda uchaguzi zote zilizofanyika tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi mwaka 1999 na hivyo mgombea wake ataonekana kukubalika kwa ajili ya uchaguzi wa mwakani.

Uchaguzi wa awali wa Nigeria ulijaa ghasia na madai ya kuwepo udanganyifu.

'Tathmini ya awali'
Bw Jonathan, aliyetoka upande wa kusini, amekuwa Rais mwezi Februari baada ya kifo cha Umaru Yar'Adua.

Awali chama hicho cha PDP kilisema mgombea wake lazima awe katoka kaskazini.

Lakini Bw Alkali ameiambia BBC chama hicho kiondoke katika 'tathmini ya awali' na badala yake ichague mgombea bora.

Alisema ratiba ya miezi minne ya uchaguzi wa awali wa chama hicho, kufanya kampeni na uchaguzi ni muda mchache sana.

Ikisema inapeleleza "nyanja zote za kisheria za kuongeza muda", tume ya taifa ya uchaguzi (Inec) imesema inabaki na msimamo wake wa kumwapisha Rais anayefuata mwezi Mei.

Bw Jonathan ameahidi kufanya marekebisho ya uchaguzi, lakini waandishi wanasema itakuwa ngumu kutekeleza mabadiliko yeyote kabla ya mwezi Januari

No comments:

Post a Comment