KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 20, 2010

Papa Benedict kuhutubia bunge Uingereza

Ziara ya kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Benedict nchini Uingereza imeingia siku ya pili, na shughuli nyingi zikifanyika jijini London.

Mambo yatakayopewa umuhimu katika siku ya pili ya ziara hiyo ni elimu inayotolewa na taasisi za kikatoliki, uhusiano wa kanisa katoliki na kanisa la Anglikana, na nafasi ya imani nchini Uingereza.
Alhamisi Papa Benedict alikutana na Malkia Elizabeth II mjini Edinburgh na pia kuongoza misa ya hadhara mjini Glasgow

Malikia Elizabeth wa Uingereza akiwa na mgeni wake Papa Benedict.Anatazamiwa kuendelea kupiga vita hali inayojiri Uingereza ya watu wengi kutotaka kujihusisha na dini, na kampeni zinazoendeshwa na makundi ya watu kama hao za kutaka imani za kidini zisitumike kama kipimo cha maadili.

Baadhi wamekuwa wakisema wazi kwamba imani za kidini ni hatari kwa uhuru na usawa katika nchi ya Uingereza.

Mbali na kuwahutubia maelfu ya watoto katika chuo cha kikatoliki cha St Mary’s magharibi mwa London, Papa Benect XVI atahutubia viongozi wa serikali na wabunge katika ukumbi wa Westminster na baadaye kufanya sala kwa pamoja na kiongozi wa kanisa Anglikana duniani Askofu mkuu Rowan Williams wa Canterbury.

Hotuba katika chuo cha St Mary’s inakusudiwa kuwa fursa ya kusherehekea kazi inayofanywa na shule za kikatoliki zaidi ya 2000 kote nchini Uingereza kwa ushirikiano na serikali.

Lakini wadadisi wanasema kwa baadhi ya watu huenda hafla hiyo ikachochea chuki dhidi ya shule zinazosimamiwa na makanisa kwa kuwa inakumbusha swala la makasisi kuwaharibu watoto.

Baadaye Papa Benedict atakutana na waakilishi wa dini nyingine kabla ya kumtembelea kiongozi wa kanisa Anglikana duniani katika makazi rasmi ya Lambeth Palace.

Mkutano baina yao utakuwa kama ishara ya maridhiano ya pande mbili hizo, kwa kuwa maaskofu wakuu wa kanisa Katoliki Uingereza waliishi kwenye makazi hayo hadi Uingereza chini ya uongozi wa mfalme Henry VIII, ilipojitenga na Rome.

Mwisho wa siku Papa Benedict alitazamiwa kuhutubia wabunge kwenye ukumbi wa Westminster

No comments:

Post a Comment