KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Monday, September 20, 2010
UN: Nchi za Afrika zimefanikiwa - MDG
Maedneleo ya Millenia
Umoja wa Mataifa umesema kuwa nchi za Afrika zimepata mafanikio kadhaa katika kupunguza umaskini kwa kipindi cha miaka kumi, tangu viongozi wa dunia walipoweka malengo ya milenia ya maendeleo.
Akizungumza mjini New York kabla ya kikao cha kutathmnini mafanikio yaliyofikiwa tangu mwaka 2000, naibu mkurugenzi wa Umoja wa Mataifa wa uhamasishaji wa malengo hayo barani Afrika Charles Aburge amesema ukuaji wa uchumi barani Afrika umesababisha kufikiwa kwa malengo hayo katika nchi nyingi.
Lakini bwana Burge ameiambia BBC kwamba Afrika inaendelea kuathiriwa chini ya kile kinachoitwa uchumi huria ambao haudhibitiwi na kodi zinazotozwa na nchi tajiri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment