KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, September 14, 2010

Simba Alipomgeuza Asusa Mkufunzi Wake


Msemo wa Simba hana urafiki na binadamu huenda ukawa na ukweli ndani yake baada ya simba mwenye uzito wa kilo 180 alipomgeukia mkufunzi wake na kujaribu kuunyofoa mguu wake.
Tukio hilo lililotokea jumatano kwenye hoteli moja mjini Los Vegas wakati wacheza sarakasi walipokuwa wakifanya shoo mbele ya watazamaji wakicheza na simba.

Ghafla simba mmoja dume alimgeukia mkufunzi wake na kuzamisha meno yake kwenye mguu wake.

Mkufunzi mwingine aliyekuwa karibu alijaribu kumzuia simba huyo asimgeuze asusa mwenzake lakini juhudi zake hazikuzaa matunda mpaka simba jike aliyekuwa pembeni alipojisogeza na kuingilia kati kumuokoa mkufunzi wake.

Video ya tukio hilo ilinaswa LIVE na wanandoa wapya waliokuwa wakila honeymoon kwenye hoteli hiyo

No comments:

Post a Comment