KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 14, 2010

Kanisa Lasisitiza Kuchoma Moto Quran Jumamosi



Pamoja na viongozi wa serikali ya Marekani na mkuu wa jeshi la Marekani kupinga kampeni ya kuchoma moto Quran, kanisa dogo la Florida, Marekani limesisitiza kuwa litachoma moto Quran siku ya jumamosi ambayo itakuwa ni siku ya ukumbusho wa septemba 11
Pamoja na kutumiwa vitisho vya kuuliwa zaidi ya 100, mchungaji Terry Jones amesisitiza kuwa kampeni yao ya kuchoma moto Quran iliyopewa jina la "International Burn-a-Koran Day" itafanyika kama ilivyopangwa jumamosi ya septemba 11.

Tukio hilo la kuchoma moto Quran litaenda sambamba na sherehe za kuadhimisha miaka 9 ya shambulizi la kigaidi nchini Marekani la mwaka 2001.

Viongozi wa serikali ya Marekani na mkuu wa majeshi ya Marekani, viongozi wa makanisa ya Marekani na marais wa nchi za Ulaya wamepinga kampeni hiyo ya kuchoma moto Quran wakisema kuwa itakuwa ni kuchochea uhasama baina ya uislamu na ukristo.

Katibu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amesema kuwa amechukizwa sana na mpango huo wa kuchoma moto kitabu kitakatifu cha Uislamu ambacho waislamu wanaamini kinatakiwa kupewa heshima kubwa sana.

Naye aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amejiunga kwenye kambi ya watu walionyanyua sauti zao kupinga uchomwaji moto wa Quran.

Kamanda wa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan, David Petraeus naye amelaani kampeni hiyo akisema kuwa itayatia majeshi ya Marekani nchini Afghanistan kwenye hatari kubwa.

Ikulu ya Marekani na makao makuu ya kanisa katoliki duniani, Vatican nao wamelaani kampeni hiyo.

Hata hivyo mchungaji Jones amesema kuwa wataichoma moto misahafu kadhaa waliyo nayo kwenye uwanja wa kanisa lao la mjini Florida linaloitwa Dove World Outreach Centre.

"Badala ya kurudi nyuma huu ndio wakati wa kusimama kidete na kutuma ujumbe wa kuupinga uislamu na kuwaambia kuwa hatutavumilia tena tabia zao", alisema Jones.

"Kama unavyoona tupo kwenye shinikizo kubwa sana la kuzivunja kampeni zetu lakini hatuna mpango wa kurudi nyuma na hivyo septemba 11 ndio siku tutakayoichoma moto Quran", alisisitiza mchungaji Jones.

Naye msemaji wa Taliban alisema: "Tunalaani vikali mpango wa kanisa la Florida kuchoma moto Quran, hii inaonyesha wanaupinga uislamu na nchi za magharibi zitajutia kwa kitendo hiki".

No comments:

Post a Comment