KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, September 17, 2010

Mwalimu kizimbani kwa kutamani mwanafunziMWALIMU Ally Msanga [39] wa Shule ya Msingi Makumbusho ya jijini Dar es Salaam, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na shitaka la kutaka kumuingilia kimwili mwanafunzi wake wa miaka 14


Mtuhumiwa huyo alipandishwa mahakamani jana Mbele ya Hakimu Susan Kihawa, na upande wa mashitaka ulikuwa ukiongozwa na Mwendesha Mashtaka, Mohamed Kilongo.

Kilongo alidai kuwa, mshitakiwa alitenda kosa hilo kati ya Mei na Septemba mwaka huu katika eneo la shule hiyo.

Kilongo alidai kuwa, mwalimu huyo alikuwa akitaka kumuingilia wmanwafunzi wake wa darasa la sita [jina linahifadhiwa] na alikamatwa wakati akitaka kumuingilia kimwili mwanafunzi huyo.

Alidai kuwa, Mei mwaka huu, mwalimu huyo alimuita mwanafuzni huyo ofisini kwa lengo la kumfanyia masahihisho kwa maswali ambayo aliyakosa kati ambayo aliyompa mwnafunzi huyo pekee na badala yake mwanafunzi huyo alipongia alianza kumshika sehemu za mwili ikiwemo na sehemu za siri.

Kilongo aliendelea kudai kuwa, Septemba mwaka huu, mshtakiwa huyo alitenda tena kosa kama hilo alimuita tena mwanafunzi huyo na kumvua sketi yake bila ridhaa kwa lengo la kumuingilia kimwili na kuonekana.

HAta hivyo Mshtakiwa alikana mashitaka hayo, na alirudishwa rumande kwa kukosa dhamana, atarudishwa tena mahakamani hapo Septemba 30, mwaka huu, kwa kesi hiyo kutajwa

No comments:

Post a Comment