KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, September 20, 2010

Obama wa Urusi Kugombea UbungeMwanaume wa nchini Azerbaijan ambaye alijipatia umaarufu mkubwa sana duniani kwa kufanana na rais wa Marekani, Barack Obama ameamua kujitosa kwenye siasa na kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi ujao nchini humo.
Asif Mustafayev ambaye zamani alikuwa msanii wa uchoraji wa picha na utengenezaji wa matangazo, alijipatia umaarufu mkubwa sana duniani kutokana na kufanana kwake na rais wa Marekani, Barack Obama.

Mustafayev ambaye amepachikwa jina la "Obama wa Azerbaijan", amepanga kuutumia umaarufu wake huo kwa kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika tarehe 7 mwezi novemba.

Mustafayev atagombea ubunge kwa kupitia chama cha DADP cha nchini humo.

Alipoulizwa kwanini amekichagua chama cha DADP, Mustafayev alisema "Obama wa Marekani alishinda urais wa Marekani kwa kupitia chama cha Democratic nami pia nimeamua kukichagua chama cha Democratic cha Azerbaijan".

Obama huyo wa Azerbaijan aliwaahidi wakazi wa jimbo lake kuwa akishinda ubunge atajitahidi kufanya kila awezalo kuliletea maendeleo jimbo lake na kuondoa utengano baina ya watu

No comments:

Post a Comment