KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 20, 2010

Ng'ombe Mdogo Kuliko Wote Duniani


Ng'ombe mdogo kuliko wote duniani kulia akiwa na ng'ombe wenye umri kama wake kushoto


Ng'ombe mdogo kuliko wote duniani amepatikana nchini Uingereza akiwa na urefu wa sentimeta 84 tu.
Ng'ombe huyo aliyepewa jina la Swallow wa Yorkshire kaskazini mwa Uingereza ameingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia, Guinness World Records akitambulika kama ng'ombe mwenye umbile dogo kuliko wote duniani.

Ng'ombe huyo mwenye urefu wa sentimeta 84 tu amezaa jumla ya watoto 9 wenye urefu wa kawaida na hivi sasa ana mimba ya mtoto wake wa 10.

Ndama wake wa tisa tayari amesharefuka sana na ana umbile kubwa kumpita mama yake.

Ng'ombe huyo mwenye umri wa miaka 11 ameingizwa kwenye kitabu cha Guinness World Records 2011 ambacho kimechapishwa leo nchini Uingereza

No comments:

Post a Comment