KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 20, 2010

'Maisha ya Jela Matamu Sana'


Mwanaume mmoja wa nchini Ujerumani alienda kwenye kituo cha polisi nchini humo akiomba arudishwe tena jela kwakuwa hakuna maisha matamu aliyowahi kuishi duniani kama maisha ya jela.
Mwanaume huyo ambaye polisi hawakumtaja jina lake alienda kwenye kituo cha polisi katika mji Saarbruecken magharibi mwa Ujerumani na kuanza kuwabembeleza polisi wamrudishe tena jela.

Mwanaume huyo alisema kuwa hajawahi kuwa na maisha matamu duniani kama wakati ambao alikuwa jela kwenye miaka ya 1980.

Mwanaume huyo baada ya kuona polisi hawana mpango wa kumtupa jela aliwauliza polisi ni kosa gani afanye ambalo litapelekea atupwe jela.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 47, aliwaonyesha polisi hati zake za kuachiwa huru kutoka jela ambako alitumikia kifungo kwenye miaka ya 1980.

Huku akiongea kwa upole katika hali ya kubembeleza, aliwaambia polisi kuwa itakuwa furaha kubwa sana kwake iwapo atafanya kosa ambalo litapelekea atupwe jela muda mrefu.

Polisi walifanya naye mahojiano kwa muda mrefu wakimshauri aache kufikiria hivyo na wamemuandalia semina ya ushauri nasaha juu ya maisha ya uraiani

No comments:

Post a Comment