KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 21, 2010

Aporwa simu mara baada ya kugongwa na baiskeliMWANAMKE mmoja jina halikuweza kupatikana, amejeruhiwa na baiskeli wakati akivuka barabara ya uhuru na punde alizungukwa na watu wakijaribu kumsaidia aliweza kuporwa simu akiwa katika mshangao.


Mwanamke huyo, aligongwa majira ya saa 4 asubuhi ya leo, maeneo ya Karume akiwa na mtoto wake Joyce [7] waligongwa kwa pamoja.

MWanamke huyo alijikuta akichanganyikiwa zaidi baada ya kuchukua mkoba wake aliyebeba mtoto wake huyo achukue simu awasiliane na ndugu yake wa karibu amfate maeneo hayo kwa dharuba iliyompata na kugundua kuwa mtoto huyo alishaporwa mfuko huo na wezi kutoweka nao.

Hata hivyo wasamaria walimshikilia mwendesha baiskeli huyo ambaye alikuwa tayari kukimbia na kumuamuru waende kituo cha polisi cha Karume kwa kuwa alimjeruhi vibaya maeneo ya usoni

No comments:

Post a Comment