KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 21, 2010

Sokwe wajifunza kukwepa mitego



Sokwe



Wawindaji kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika hutumia mitego kwa ajili ya kunasa wanyama pori kwa kitoweo, mitego hii ikiua au kumjeruhi mnyama yule.

Hata hivyo kuna baadhi ya masokwe wanaoishi katika misitu ya Guinea ambayo wamejifunza jinsi ya kutambua mitego hii, kwa mujibu wa wataalamu wanaofanya utafiti kuhusu nyenzo na tabia ya sokwe.

La kustaajabisha ni kwamba sokwe hawa hujitahidi kutafuta na kuiharibu mitego bila madhara.

Ugunduzi wa tabia ya sokwe hawa ulifanywa na wataalamu wa masuala ya wanyama pori Bw Gaku Ohashi na Tetsuro Matsunzawa waliokuwa wakifuatilia tabia na nyenzo za sokwe huko Bossou nchini Guinea.

Kuna ripoti nyingi za kujeruhiwa kwa sokwe wengi Afrika mashariki na magharibi kukisababishwa na mitego ambapo wengi wamekufa ndani ya mitego hiyo.

Hata hivyo, kuna taarifa chache kuhusu kujeruhiwa kwa sokwe wanaopatikana huko Bossou, jambo linaloshangaza kwa sababu sokwe hawa wanaishi karibu na makaazi ya watu ambako mitego hutumiwa mara kwa mara




Masokwe

Wataalamu wamegundua sababu
Wakati wakifanya utafiti wao, Bw Ohashi na Prof Matsuzawa kutoka kitivo cha uchunguzi wa wanyama pori cha Chuo Kikuu cha Kyoto, Japan, waligundua kuwa sokwe watano wa kiume wenye umri mdogo na mmoja mkubwa walikuwa wanajaribu kuvunja na kuinasua mitego kadhaa.




Kwa mara mbili wataalamu hawa walishuhudia sokwe hawa wakifanikiwa kuinasua mitego iliyowekwa kuwanasa wao.





Sokwe

Nyaya
Mtego wa kawaida, kwa mfano unaotengenezwa na kabila la Manon wa huko Bossou, huundwa kwa waya wa chuma unayozungushwa kamba ya mimea ya msituni.

Nyaya hizi hazibagui ni mnyama gani anayenaswa.

Lakini sokwe wa kiume wa Bossou wamegundua jinsi ya kukwepa njama za wawindaji wa huko.

Kwa mujibu wa Bw Ohashi alipozungumza na BBC alisema kuwa sokwe hawa ni kama wanafahamu sehemu yenye hatari na sehemu ambazo hazina tatizo na hivyo kufanikiwa kujiondolea hatari.

Mara nyingi sokwe hawa walishika kijiti cha mtego na kukitikisa kwa nguvu hadi mtego ukaachia na mara nyingine hugonga kijiti kinachoshikilia mtego na kusubiri kiachilie kisha huvunja mtego mzima.

Hii ndiyo ripoti ya kwanza kuhusu sokwe wanaovunja na kuharibu mitego iliyokusudia kuwanasa.



Vile vile kitendo cha sokwe hawa kinaelezea kuwa sokwe wanaweza kujifunza na kufahamu.



Mara nyingi sokwe hujifunza kwa kujaribu bila kujali athari yoyote. Mfano ni wanapojaribu kuvunja mbegu, hutumia jiwe na wanapokosea hujaribu kutumia mikono bila kufanikiwa.

Majaribio ya aina hiyo hayangeweza kufanikishwa juu ya mitego, sababu kosa moja lingesababisha kifo. Kwa hiyo ina maana kuwa sokwe wanaweza kujifunza na kutumia mbinu ambayo haihatarishi maisha yao, alisema Bw.Ohashi.

Wakati wote huu, sokwe wachanga walifuatilia jinsi sokwe mkuu anavyofanya kabla ya kusogelea mtego ule na kuugusa baada ya kuhakikisha kuwa ni salama kufanya hivyo.

Wataalamu hawa wanasema kuwa mitego hii ni tishio kubwa kwa sokwe na wanaongoza juhudi za kuchambua misitu ili kuondoa mitego yote iliyoko.

Wanasema pia kwamba sokwe kutoka maeneo mengine hawajafikia kiwango cha wenzao wa Guinea katika kuondoa hatari inayowakabili ya mitego ya wawindaji

No comments:

Post a Comment