KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, September 14, 2010

Kesi ya Rama yahamishiwa Mahakama Kuu

BAADA ya upelelezi kwa upande wa mashitaka kukamilika, kesi ya mauaji inayomkabili Ramadhan Mussa (18) na mama yake, Hadija Selemani (38) kesi hiyo iko tayari kwa kuanza kusikilizwa Mahakama Kuu.


Katika kesi hiyo jumla mashahidid 17 na vielelzo sita vitatumika kusikilizia kesi hiyo katika mahakama hiyo.
Vielelezo hivyo vikiwemo ripoti ya mkemia mkuu kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na tariofa ya ulinzi ktuoka serikali za mtaa anakoishi mtuhumiwa huyo.

Wakili Beatha Kitaku aliwasilisha maelezo hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi Waliarwande Lema wa Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa maelezo ya awali jana.

Rama na mama yake wanakabiliwa na makosa ya mauaji baada ya kudaiwa kuwa, Aprili 25, mwaka juzi, majira ya usiku, huko maeneo la Tabata Segerea Kwa Bibi washtakiwa hao walimuua mtoto Salome Yohana.

Mshitakiwa Rama alikutwa na kichwa cha mtoto hiuyo katika hospitali ya Taifa Muhimbili na kukamatwa


Awali mshitakiwa Rama alipandishwa kizimbani kwa kesi hiyo akiwa na umri wa miaka 16

No comments:

Post a Comment