KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, September 23, 2010

Mwizi Anapopitiwa na Usingizi Kwenye Nyumba Anayoiba..


Polisi nchini Malaysia wamemtia mbaroni mwizi ambaye alizamia kwenye nyumba ya mtu kuiba na kupitiwa na usingizi kwenye kochi la nyumba hiyo aliyoingia kuiba.
Polisi wa nchini Malaysia wamemtia mbaroni mwizi ambaye alivunja na kuingia kwenye nyumba ya mtu kuiba na bila kutegemea alipitiwa na usingizi kwenye kochi huku vitu alivyotaka kuviiba vikiwa pembeni yake.

Kwa mujibu wa polisi, mwizi huyo mwenye umri wa miaka 42 alizamia kwenye nyumba moja katika jimbo la Penang kaskazini mwa Malaysia na kuiba saa na vito vya thamani.

Taarifa ya polisi ilisema kuwa kulikuwa hakuna mtu ndani ya nyumba hiyo wakati kibaka huyo alipoingia ndani kwani wakazi wa nyumba hiyo walikuwa wameenda vakesheni.

Waliporudi walishangaa kuona sebule yao ikiwa imevurugwa vurugwa na mwizi huyo akiwa amelala kwenye kochi huku vitu alivyotaka kuviiba vikiwa pembeni yake, liliripoti gazeti la New Straits Times.

Mwizi huyo alikurupuka na kukimbia kupitia dirishani baada ya kuamshwa na kuwaona wakazi wa nyumba hiyo wakiwa wamesimama mbele yake.

Hata hivyo hakufika mbali alikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi, mkuu wa polisi wa wilaya ya Penang alithibitisha tukio hilo.

Vitu alivyotaka kuiba vilikuwa na thamani ya dola 3400

No comments:

Post a Comment