KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, September 23, 2010
Chaja za Simu na Laptop Zisizohitaji Umeme
Siku za kutafuta umeweka wapi chaji yako ya simu au kujikwaa kwenye waya wa chaja ya simu zitakuwa ni historia ndani ya miaka miwili ijayo baada ya kugunduliwa kwa njia ya kuchaji simu au laptop bila kuhitaji waya wa kuchomekwa kwenye umeme.
Ndani ya miaka miwili ijayo watu wataweza kuchaji simu, laptop zao na vifaa vingine vya umeme bila ya kuhitaji waya wa kuunganisha kwenye umeme kwani kampuni ya teknolojia ya Fujitsu imegundua njia ya kuchaji betri bila kutumia waya wa umeme "Wireless Charging".
Kampuni hiyo ya Japan imetumia teknolojia ya sumaku kuweza kutengeneza mfumo wa kuchaji betri bila kutumia waya ambao utaingia madukani ndani ya miaka miwili ijayo.
Kifaa kinachotumia mfumo huo kitawawezesha watu kuchaji vifaa vingi kwa wakati mmoja kama vile, simu, kamera na laptop bila ya kuhitaji waya wowote wa kuchomeka kwenye umeme.
Kifaa hicho pia kitawawezesha watu kuchaji vifaa vyao vya umeme wakiwa mbali kama ambavyo watu wanavyotumia wireless internet.
Ugunduzi huu utapelekea migahawa na sehemu mbalimbali zenye mkusanyiko wa watu kuweka maeneo ya watu kuchaji vifaa vyao vya umeme kama ambavyo baadhi ya migahawa inavyotoa wireless ya bure kwa wateja wao.
Mbali ya umbali na kutohitaji waya wowote, kampuni ya Fujitsu ilisema kuwa vifaa vyao vina uwezo wa kuchaji vifaa vya umeme kwa haraka zaidi mara 150 zaidi ya ilivyo sasa.
Hata hivyo Fujitsu haijasema kuwa vifaa hivyo vitauzwa bei gani vitakapoanza kuuzwa mwaka 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment