KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, September 20, 2010

Mkemia Mkuu afariki, maiti yake yakutwa Hotelini


MKEMIA Mkuu wa Serikali, Ernest Mashimba amefariki dunia juzi mkoani Tanga, wilayani Lushoto ambapo mwili wake umekutwa katika chumba cha Hoteli aliyofika iitwayo Executive Lodge iliyopo wilayani humo.
Imedaiwa kuwa Mashimba alikuwa amekwenda wilayani kwa lengo la kuhudhuria mahafali ya shule ya Sekondari Kifungilo ambapo alikuwa ni mmoja kati ya wazazi na aliteuliwa na uongozi wa shule kusoma risala maalum kwa wahitimu katika mahafali hayo.

Kifo hicho kilibainika Jumamosi asubuhi katika hoteli hiyo baada ya wahudumu kushitushwa na kiongozi huyo kuchukua mdua mrefu bila kuonekana akitoka chumbani humo na uongozi walipochukua uamuzi wa kufungua mlango huo walimkuta kitandani akiwa tayari ameshafariki dunia muda mrefu ..

Mashimba alikwenda mkoani humo kuhudhuria mahafali na uongozi wa shule hiyo kumteua asome risala kwa niaba ya wazazi wenye watoto shuleni hapo na badala yake aliteuliwa mzazi mwingine baada ya kupewa taarifa kuwa amefariki .

Mkuu wa wilaya ya Lushoto Bi. Sophia Mjema alisema chanzo kilichofanya mkuu huyo kufariki dunia bado hakijafahamika na kitafahamika baada ya uchunguzi

No comments:

Post a Comment