KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 20, 2010

Hatma ya kocha wa Togo yatolewa




Uchunguzi ulianza kufanyika baada ya mechi ya Septemba 7
Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Togo amesimamishwa kazi kwa miaka mitatu baada ya kuandaa mechi bandia huko Bahrain mapema mwezi huu.

Shirikisho la mpira la Togo limesema Tchanile Bana aliandaa mchezo wa kirafiki na Riffa, bila ya chombo hicho cha kusimamia soka kupewa taarifa.

Kundi la wachezaji liliojifanya kama timu ya taifa lilishindwa kwa mabao 3 kwa bila.

Bw Bana tayari alishasimamishwa kwa miaka miwili kwa kuandaa mechi bandia dhidi ya Misri mwezi Julai.

Shirikisho hilo la soka limesema katika taarifa yake, " Uandaaji na usimamizi wa mechi hiyo ulipangwa na Tchanile Bana".

Antoine Folly, mwanachama wa tume ya nidhamu, alisema wengine wote waliohusika nao pia lazima wachukuliwe hatua.

Alisema, " Suala hili la Bahrain lazima lifuatiliwe kwa makini ili kufichua na pia kuweka vizuizi kwa alioshirikiana nao ndani ya shirikisho la soka la Togo".

Mamlaka za soka za Togo zilianza kufanya uchunguzi baada ya ripoti za mechi dhidi ya Bahrain, kufanyika katika uwanja wa taifa huko Riffa Septemba 7

No comments:

Post a Comment