KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 20, 2010

Karibu tena yamponza mfanyabiashara


MFANYABIASHARA aliyejitambulisha kwa jina moja la Saimon, jana alijikuta yupo kwenye wakati mgumu baada ya kutumia lugha ya 'karibu tena'na mteja huyo kupokea ukaribisho huo kinyume.
Mfanyabiashara huyo anayefanya shughuli zake maeneo ya Keko ambapo anajishughulisha na uuzaji wa masanduku ya kubebea miili mfu “majeneza” alijikuta yupo kwenye wakati mgumu baaada ya mteja wake huyo kumtupia maneno makali kuashiria hakupenda alichoambiwa na mfanyabiashara huyo.

Mfanyabiasha huyo alikutwa na dhahama hiyo baada ya kuwauzia jeneza moja la mtoto, familia moja iliyofika katika ofisi hiyo na kukubaliana bei na badala ya kumalizana mafanyabiasha huyo aliwakariisha wateja wake hao kwa kuwaambia karibuni tena tendo ambalo wateja hao hawakupenda ukaribisho huo.

Chanzo chetu cha habari kilidai kuwa, walifika kununua jeneza hilo alikuwemo kijana mmoja, na wanaume wengine wamakamu na kijana huyo alianza kumtolea maneno makali mfanyabiashara huyo kuwa hakupaswa kumkaribisha kwa kuwa alikuwa akimuombea mabaya.

Kilidai kuwa, “watu wamefiwa, unapomwambia karibu tena ina maana gani, alihoji kijana huyo kwa jazba na mfanyabiashara huyo kuwa mpole kwa kukiri kufanya kosa kutumia lugha hiyo.

Hata hivyo ilidawa kuwa wateja wengi wafikao mahali hapo huwa hawapendi kuambiwa lugha hiyo na wafanyabiashara wengi huwa hawatumii liugha hiyo

No comments:

Post a Comment