KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, September 17, 2010

Midahalo haina faida -KinanaCHAMA CHA MAPINDUZI kimewapiga marufuku wagombea wake wa ubunge nchini kote wasishiriki katika midahalo inayoendeshwa na kuandaliwa shirika la utangazaji [TBC].
Katazo hilo lilitolewa na kutangazwa na katibu mkuu wa chama hicho, Yusuph Makamba na kutoa taarifa hiyo kwenye chombo hicho kuwataka wagombea wa chamda hicho wasishiriki midahalo inayoandaliwa na kituo hicho hadi watakapotoa tamko maalum.

MAkamba alisema, wamewasimamisha wagombea wake wasishiriki midahalo hiyo na wataanza kushiriki hadi watakaporuhusiwa.

TBC imeandaa kipindi maalumu cha kutembelea kila jimbo kwa kuwakutanisha wagombea wa jimbo hilo na wapiga kura wao na kumwaga sera zao mbel ya wapiga kura hao.

Nae meja wa kampeni wa Chama Cha CCM, Abrahamani Kinana alipotakiwa kufafanua ni kwanini waliwazuia wagombea wao alisema, haoni faida ya midahalo hiyo kwa chama hicho kwa kuwa muda huu CCM ina muda wa kutangaza sera zao na kuongeza kuwa midahalo hiyo imetawaliwa na malumbano majukwaani

No comments:

Post a Comment