KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, September 16, 2010

Kanisa kusaidia waathirika wa ulawiti

Mkuu mpya wa Kanisa Katoliki wa Ubelgiji, ameahidi kuwasaidia walioathirika na tuhuma za kulawiti vijana, katika jitihada zake za kurejesha imani kwa jamii.





Askofu mkuu Andre Joseph Leonard amesema ingawa Kanisa hilo halitakuwa na uwezo wa kutoa suluhu ya mara moja,litaunda kituo cha kuwasaidia walioathirika.

Tume huru iliyochunguza tuhuma hizo iligundua kuwa vitendo hivyo vilifanyika katika kila dayosisi katika kipindi cha miaka mingi.

Watoto wachanga
Tume hiyo imesema baadhi ya waathirika walikuwa watoto wachanga wakati vitendo hivyo vikianza.

"Itabidi tusikilize hoja zao, kurejesha utu wao na kuwasaidia kupunguza machungu yaliyowapata"

Askofu Mkuu huyo amesema Kanisa Katoliki litatoa "nafasi za kutosha" kwa waathirika wa vitendo vya ulawiti.
"Itabidi tusikilize hoja zao, kurejesha utu wao na kuwasaidia kupunguza machungu yaliyowapata," amesema.

"Tunataka kujifunza kutokana na makosa. Mitazamo na majumuisho ndani ya uchunguzi huo yatafanyiwa kazi," ameongeza Askofu Mkuu.

Itabidi tusikilize hoja zao, kurejesha utu wao na kuwasaidia kupunguza machungu yaliyowapata

Askofu MkuuAndre-Joseph Leonard

Amesema kanisa hilo linataka kituo cha "utambuzi, maridhiano na uponyaji", lakini kutokana na ukubwa wa jambo lenyewe, kituo hicho hakitakuwa tayari kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Amesema kanisa linataka kushirikiana kwa karibu na polisi wanaofanya uchunguzi wa tuhuma za ulawiti, lakini hakutoa maelezo yoyote ya jinsi jambo hilo litakavyofanyika.

Aidha amewaonya wale wanaohusika kuwa watakabiliwa na vikwazo kwa mujibu wa sheria za canon, ikiwemo kuondolewa kabisa katika kanisa.

Maswali mengi

Mmoja wa watu katika kundi la walioathirika amesema hatua ya kuanzisha kituo kama hicho, ambacho kinaendeshwa na kanisa haitoshi. "Hakuwezi kuwa na tume ya uchunguzi inayochunguza uhalifu uliofanyika ndani taasisi inayoendeshwa na taasisi yenyewe," amesema msemaji wa kundi la waathirika la Droits de l'Homme dans l'Eglise.

Jitihada za kutafuta suluhu juu ya sakata la vitendo vya ngono zilizolitikisa Kanisa Katoliki nchini Ubelgiji, linatoa maswali mengi kuliko majibu, anasema mwandishi wa BBC Jontly Bloom mjini Brussels



Machungu waliyoyapata



Ikiwa kanisa linataka kumaliza kabisa jambo hili mara moja, basi litakuwa limekosea, amesema mwandishi wa BBC.


Kiwango,kiasi na muda wa vitendo hivyo, ambayo vilitangazwa wiki iliyopita, kimewashitusha hata wajumbe wa tume iliyoundwa na kanisa kufanyia uchunguzi tuhuma hizo, ameongeza mwandishi huyo.

Wasichana 100

Tume hiyo iligundua kuwa vitendo hivyo vilifanyika chini ya mapadre, walimu, wafanyakazi na katika tukio moja askofu, na vitendo vyenyewe kufikia 300.

Tume inayochunguza imesema haijakuta ushahidi wowote wa mpango wa kuficha vitendo hivyo. Vyombo vya habari vya Ubelgiji vimelituhumu kanisa kwa kuficha unyanyasaji huo licha ya watuhumiwa kushitakiwa.

Theluthi mbili ya waathirika ni wavulana, lakini wasichana 100 pia waliathirika. waathirika wapatao 13 walijiua kutokana na hilo.


Kituo cha maridhiano kitajengwa mahala ilipokuwepo tume ya uchunguzi ambayo ilifungwa baada ya polisi kuvamia na kuchukua majalada mapema mwaka huu. Mahakama ya rufaa ilitoa uamuzi wiki iliyopita kuwa uvamizi huo wa polisi ulikuwa kinyume cha sheria, na majalada yalitochukuliwa hayawezi kutumika na waendesha mashitaka.


Waathirika wengi walijitokeza na kutoa ushuhuda wao mbele ya tume hiyo baada ya askofu wa Bruges, Roger Vangheluwe kujiuzulu mwaka huu, baada ya kukiri kumlawiti mtoto mmoja, kabla na baada ya yeye kuwa askofu

No comments:

Post a Comment