KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, September 20, 2010

Mama amchana mwanae viwembe kwa wizi


FATUMA Rashid [27] mkazi wa Buguruni, jana amejikuta akipandwa na hasira kali na hasira hizo zilimfanya akimbilie dukani na kununua wembe aina ya Gillete na kumpa adhabu mwanae aliyegundua kuwa amechukua pesa ndani bila ridhaa yake.
Fatuma alichukua uamuzi huo baada ya kukerwa na tabia hiyo ambayo alikuwa hafahamu ni mtoto wake yupi anachukua pesa hizo na huku kila akiwauliza huwa wanakiri kuwa hawahusiki na uchukuaji wa pesa hizo.

Hivyo jana majira ya mchana, alimbaini mtoto wake wa kiume 9 alichukua shilingi elfu mbili ambayo aliiweka kwa lengo la mtego kumbaini na mdokoaji huyo.

FAtuma a lipobaini mtoto wake huyo alichukua pesa hiyo, hakutaka ushauri na kuchukua uamuzi wa kumchanjachanja vidole vyake anavyotumia kuchukua pesa hizo kwa lengo la kumuadhibu

No comments:

Post a Comment