KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 20, 2010

Mtoto Akutwa Kwenye Choo Cha Ndege


Mtoto mchanga wa kiume amekutwa akiwa hai kwenye pipa la taka la kwenye choo cha ndege iliyowasili nchini Philippines ikitokea Bahrain.
Kwa mujibu taarifa zilizotolewa punde baada ndege ya shirika la ndege la Gulf Air kutua mjini Manila, Philippines ikitokea Bahrain, wafanya usafi waliingia kwenye ndege hiyo baada ya abiria wote kushuka na ndipo walipokumbana na tukio wasilolitegemea baada ya kumkuta mtoto mchanga aliyezaliwa muda mfupi uliopita akiwa kwenye pipa la taka la chooni.

Mtoto huyo mchanga wa kiume alikuwa amezungushiwa makaratasi ya chooni akiwa bado hajasafishwa damu toka kwenye mwili wake huku kipande kikubwa cha utambi wa kitovu kiking'inia.

Madaktari waliitwa na kumchunguza mtoto huyo na kutoa taarifa mtoto huyo bado yuko hai na mwenye afya njema.

Mtoto huyo alipewa jina kwa kutumia herufi mbili za GF zinazowakilisha Gulf Air pia herufi hizo ziliwakilisha jina jingine alilopewa la George Francis.

Mtoto huyo wa kiume alisafishwa kwa kutumia maziwa na manesi wa uwanja wa ndege mjini Manila.

Polisi wanafanya uchunguzi kumtafuta mama wa mtoto huyo ambaye aliwashangaza watu kwa jinsi alivyoweza kujifungua mwenyewe ndani ya ndege bila ya kushtukiwa na mtu yeyote.

Kwa mujibu wa polisi wa Manila, mama huyo akipatikana atafunguliwa mashtaka mahakamani

No comments:

Post a Comment