KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 13, 2010

Korea kaskazini yaahirisha mkutano wa chama tawala
PYONGYANG

Televisheni ya Korea Kusini inaripoti kwamba mkutano muhimu wa chama tawala nchini Korea Kaskazini, umeahirishwa kwa sababu ya tetesi kwamba kiongozi wake Kim Jong-Il anakabiliwa na matatizo ya afya. Ikivunukulu vyanzo vya ujasusi nchini Korea Kusini, televisheni hiyo inasema hali ya afya ya Kim Jong Il mwenye umri wa miaka 68 ilizidi kuwa mbaya baada ya ziara yake ya siku tano kaskazini mashariki mwa China mwezi uliopita. Inadhaniwa kiongozi huyo alipigwa na kiarusi mnamo mwaka 2008.

Mkutano wa chama tawala cha Wafanyakazi, uliotangazwa tangu mwezi Juni mwaka huu, na ambao ungekuwa mkutano mkubwa na muhimu wa kisiasa kuwahi kufanyika katika kipindi cha miaka 30, ulitarajiwa kumfungulia njia mwanawe mdogo Kim, Kim Jong-Un hatimae kuchukua madaraka.

No comments:

Post a Comment