KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 13, 2010

Benki kutakiwa kuongeza mitaji




BASEL

Wasimamizi wa masuala ya fedha duniani wamekubaliana kuhusu sheria mpya zinazonuiwa kuimarisha akiba za benki ili kuzuia kutokea tena mzozo wa fedha kama ule wa mwaka 2008. Sheria hizo mpya, zilizopitishwa kwenye mkutano uliofanyika jana mjini Basel, Uswisi, zitazitaka benki kuweka akiba ya mitaji ya asilimia saba ya kiwango jumla cha fedha inazokopesha.

Kiwango hiki kipya kinakaribia mara tatu zaidi kuliko kiwango cha chini cha hapo awali, na kinalenga kuhakikisha benki zinaweza kulipa gharama za madeni yasiyoweza kulipwa. Mkuu wa benki kuu ya Ulaya, Jean-Claude Trichet, amelipongeza pendekezo hilo akisema litatoa mchango muhimu kuimarisha uthabiti wa kifedha na ukuaji wa kiuchumi katika kipindi cha muda mrefu.

Viongozi wa nchi 20 tajiri duniani watayajadili mapendekezo hayo kwenye mkutano wao uliopangwa kufanyika mjini Seoul, Korea Kusini, mwezi Novemba mwaka huu

No comments:

Post a Comment