KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 14, 2010

Hatimaye Kanisa Laahirisha Kuchoma Moto QuranMchungaji Terry Jones na kanisa lake la watu 50 la Florida nchini Marekani hatimaye ameamua kuahirisha mpango wake wa kuchoma moto Quran siku ya jumamosi baada ya shinikizo kubwa toka kwa viongozi wa juu wa Marekani akiwemo rais wa Marekani, Obama
Mchungaji Terry Jones wa kanisa dogo la Dove World Outreach Center la mjini Gainesville, Florida nchini Marekani ameahirisha mpango wake wa kuchoma moto Quran siku ya jumamosi ambayo ni siku ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha yao kwenye shambulio la kigaidi la septemba 11 mwaka 2001.

Akitoa tamko la kuahirisha kampeni yake ya kuchoma moto Quran ambayo imekuwa ikilaaniwa na viongozi wa dini na serikali nchini Marekani, Mchungaji Jones akiambatana na imamu wa Florida, alisema kuwa ameamua kuahirisha mpango wake huo baada ya kufikia muafaka na imamu wa Florida kuwa imamu wa New York na wahusika wa ujenzi wa msikiti ulio karibu na eneo la Ground zero ambalo majengo ya Twin Tower yaliporomoshwa, wamekubali kuuhamisha msikiti huo.

Hata hivyo muda mfupi baada ya kutoa tamko hilo, imamu wa New York, Feisal Abdul Rauf alitoa tamko akisema kuwa hajazungumza na mchungaji Jones wala imamu wa Florida, Muhammad Musri na hakuna makabuliano yoyote ya kuuhamisha msikiti ulio karibu na Ground zero.

Imamu Musri alithibitisha baadae kuwa hakuzungumza na Imamu wa New York na hakuna makubaliano yaliyofikiwa kuuhamisha msikiti huo.

Mchungaji Jones alisema kuwa yeye na imamu Musri wataenda New York jumamosi kukutana na imamu wa New York, lakini taarifa zilisema imamu wa New York hana mpango wa kukutana na mchungaji Jones.

Awali Rais wa Marekani, Barack Obama alitoa hotuba akisema kuwa kitendo cha mchungaji Jones kitahatarisha maisha ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.

"Hii ni sawa na bonanza ya ajira kwa Al-Qaeda, kutatokea ghasia nyingi sana katika nchi kama Pakistan na Afghanistan, tukio hili litapelekea kuongezeka kwa idadi ya watu watakaojitolea kujilipua kwenye miji ya Marekani na barani ulaya", alisema Obama akimuonya mchungaji Jones aahirishe mpango wake huo wa kuchoma moto Quran.

Wakati huo huo Taliban nchini Afghanistan wameanza kusambaza vipeperushi nchini humo vinavyosema kuwa Marekani ni adui mkubwa wa uislamu

No comments:

Post a Comment