KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, September 16, 2010

Nadal Ashinda Marekani




Rafael Nadal ameingia katika orodha ya miamba ya wacheza tennis duniani baada ya kumshinda Novak Djokovic kwenye michuano ya wazi ya Marekani (US Open).


Rafael Nadal


Mhispania huyo, mwenye umri wa miaka 24, alishinda katika mchezo wa fainali uliozongwa na mvua kwa seti 6-4 5-7 6-4 6-2, kwenye viwanja vya Flushing Meadows jijini New York.

Ushindi huu wa kwanza wa michuano ya wazi ya Marekani umemfanya Nadal kufikisha taji la tisa la michuano mikuu ya tennis duniani.

Na ushindi huo unamfanya kuwa mchezaji wa saba katika historia kunyakua ushindi wa michuano mikuu ya Wimbledon, ya Ufaransa, Australia na Marekani.

Nadal anaungana na Roger Federer, Andre Agassi, Roy Emerson, Rod Laver, Don Budge na Fred Perry walioweza kunyakua mataji makuu duniani. Aidha pia anakuwa mchezaji wa kwanza, tangu Laver mwaka 1969 kushinda michuano ya Ufaransa, Wimbledon na Marekani katika mwaka mmoja.

No comments:

Post a Comment