KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 13, 2010

Kampeni za uchaguzi zasitishwa Guinea Conakry
CONAKRY

Serikali ya mpito nchini Guinea imesitisha kampeni za uchaguzi kufuatia machafuko ya siku mbili yaliyozuka kati ya wafuasi wa wagombea wawili katika uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Jumapili ijayo. Mtu mmoja aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kwenye machafuko hayo yaliyozuka mwishoni mwa juma lililopita. Waziri mkuu wa zamani wa Guinea Conakry, Cellou Dalein Diallo anapewa nafasi kubwa ya kushinda duru ya pili ya uchaguzi wa rais baada ya kupata zaidi ya mara mbili ya kura alizopata mpinzani wake, Alpha Conde kwenye duru ya kwanza.

Wagombea hao wanakutana leo na rais wa mpito, Sekouba Konate, kujadili machafuko hayo yanayoelezwa kuwa pigo kwa uchaguzi unaonuiwa kuuwezesha utawala wa kijeshi kukabidhi madaraka kwa rais atakayechaguliwa.

No comments:

Post a Comment