
LONDON
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limechapisha ripoti hii leo likisema watu takriban 30,000 nchini Irak

wamehukumiwa vifungo gerezani bila kufunguliwa mashtaka wala kuwa na wakili. Shirika hilo linasema wafungwa wanakabiliwa

na kitisho kikubwa cha mateso na kutendewa vitendo vibaya.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo shirika la Amnesty International linasema maafisa wa Irak wanawazuilia wafungwa wasio rasmi

katika magereza ya siri na watu kadhaa wamekufa kutokana na mateso gerezani. Katika ripoti hiyo, iliyopewa jina "Enzi mpya ya utawala

mateso yale yale" shirika hilo linaitaka serikali ya Irak kuwalinda vyema zaidi wafungwa.
No comments:
Post a Comment