KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 14, 2010

Amtukana Obama, Afungiwa Maisha Kwenda MarekaniKijana wa Kiingereza ambaye alimtumia rais wa Marekani email ya vitisho na kashfa amefungiwa maisha kuingia Marekani.
Luke Angel alifuatiliwa na polisi wa Marekani na Uingereza baada ya kumtumia email ya vitisho na kashfa rais wa Marekani, Barack Obama na kumfananisha rais huyo wa taifa kubwa duniani na sehemu za siri za kike.

FBI waliichunguza email ya Luke na kisha kuwajulisha polisi wa Uingereza ambao waliendaaa nyumbani kwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 anayekaa Silsoe, Bedfordshire.

Luke, ambaye ni mwanafunzi wa sekondari, ameingia kwenye orodha ya watu waliopigwa marufuku kukanyaga ardhi ya Marekani maishani.

Luke aliliambia gazeti moja la Bedfordshire kuwa aliamua kumtumia Obama email hiyo ya kashfa baada ya kuangalia kipindi kwenye luninga kilichokuwa kikizungumzia shambulizi la kigaidi la septemba 11,2001.

"Polisi walikuja nyumbani kwetu na kunipiga picha na kuniambia kuwa nimepigwa marufuku kuingia Marekani", alisema Luke.

"Sijali kupigwa marufuku kuingia Marekani ingawa wazazi wangu hawajafurahia", aliongeza Luke.

Polisi hawana mpango wa kumfikisha mahakamani kijana huyo.

No comments:

Post a Comment