KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, September 23, 2010

Mengi amwaga Milion 13 Kwa Wanafunzi AzaniaMWENYEKITI Mtendaji wa IPP, Bw. Reginald Mengi, amekabidhi hundi ya Shilingi. milioni 13 kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Azania ya jijini Dar es Salaam waliofaulu na kupata daraja la kwanza katika mitihani yao ya kidato cha sita ya mwaka j
Mengi alitoa zawadi hiyo kwa wanafunzi hao ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyowapa wanafunzi hao alipotembelea shule hiyo Februari mwaka huu katika mahafali ya wanafunzi hao na kuwaahidi atamzawadia kila mwanafunzi kiasi cha shilingi milioni moja kila mmoja atakayefanya vizuri mitihani hiyo.

Mbali na kutoa hundi hiyo kwa wanafunzi hao Mengi aliweza kuwapatia nauli wanafunzi wanaotoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam

Akitoa hundi hiyo Mengi alipongeza wanafunzi hao kwa ushindi wao na kuwataka wasijiamini kama wameshinda maisha na kuwataka wakaze msuli zaidi katika masomo yao yajayo na wasibweteke dhidi ya ushindi huo.

Pia aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa kuwa bila ya juhudi ya walimu hao wasingeweza kutoa matokeo hayo na kusema mafanikio waliyoyapata wanafunzi hao yametokana na ubora wao wa kufundisha.

Wanafunzi waliokabidhiwa hundi hizo ni Abdallah Shabani, Elifuraha Msese, Fuad Shaibu, Acky Charles, Charles Otto, Geofrey Jacob, Hosea Chamba, Laban Kebacho, Shabani Mzee, Mohamed Said, Raymond Shelukindo, na Shadrack Lusasi

No comments:

Post a Comment