KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Tuesday, September 21, 2010
Wenye kumbi wapewa miezi mitatu kusajili kumbi zao
WIZARA ya Habari, Utamaduni na Michezo imetoa muda wa miezi mitatu kwa wamiliki wa kumbi za starehe wawe wamesajili kumbi zao na watakaokiuka hatua kali dhidi yao zitachukuliwa.
Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, ya Bw.Ceth Kamuhanda wakati alipokuwa akizungumza
kwenye mdahalo maalum wa jukwaa la Sanaa.
Alisema wenye kumbi watatakiwa kusajili kumbi zao kwa kuwa kumekuwa na ukiukwaji wa makusudi wa
Sheria,kanuni na taratibu za kuendesha kumbi hizo na kusababiusha kuleta maafa kwa watumiaji wa kumbi hizo.
Alisema sifa za kumbi zinazokubalika kisheria ni pamoja na kuwa na milango ya kutosha inayofungukia nje,vyoo nadhifu vya wanawake na wanaume, miundombinu kwa walemavu, vifaa vya kuzimia moto, maegesho ya vyombo vya usafiri na ulinzi kamili na wauhakika.
Pia alisema kumbi zote lazima zisajiliwe Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Hivyo hadi ifikapo Desemba 31, mwaka huu wamiliki hao wanatakiwa wafike BASATA wasajili kumbi zao na kinyume na hapo msako mkali utafanyika kubaini wanaoendesha kumbi hizo kiholela
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment