KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, August 24, 2010

Yu hatihati kufanya mtihani

MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar e salaam, anakabiliwa na hatihati ya kutofanya mtihani wake wa kidato cha nne kutokana na kusumbuliwa na ujauzito alionao.

Mwanafunzi huyo [jina kapuni] ambaye amekuwa mahudhurio yake yanazidi kufifia siku hadi siku kutokana na ujauzito huo kukua na kushindwa kumudu masomo yake ipasavyo.

NIFAHAMISHE ilibahatika kumuona mwanafunzi huyo ambaye anaonekana kuchoka na hata kushindwa kuhudhuria vipindi darasani na kujikuta akilala ndani ya maeneo ya shule kwa kuchoshwa na ujauzito huo.

AWali mwanafunzi huyo kabla hajagundulika shuleni hapo alikuwa akificha hali yake hiyo na hatimaye aliweza kugundulika kwa kushindwa kuidhibiti hali hiyo.

MArafiki wa karibu na msichana huyo walidai kuwa mwenzao huyo mahudhurio yake yalikuwa ni finyu kwa kukabiliwa na tatizo hilo .

No comments:

Post a Comment