KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, August 24, 2010

HUZUNI vilitawala katika mazishi ya aliyefariki dunia kwa sababu iliyodaiwa ni kutokana na mapaka


HUZUNI vilitawala katika mazishi ya aliyefariki dunia kwa sababu iliyodaiwa ni kutokana na mapaka yaliyokuwa yakilia usiku kucha katika nyumba yao.
Katika mazishi hayo majirani, ndugu na jamaa waliohudhuria mazishi walitawaliwa na masikitiko kutokana na kijana huyo kufariki ghafla kwa kuugua kwa muda wa siku moja na kupelekea ndugu waliobaki katika nyumba hiyo kubaki na hofu.

Ilidaiwa na ndugu wa karibu wa marehemu huyo kuwa ndugu yao huyo huenda kifo chake kimesababishwa na mkono wa mtu kwa kuwa ndugu yao hakuwa mgonjwa awali kabla ya matukio hayo ya paka.

“Tunahusisha kifo chake na wale paka ambao walikuwa wanakuja nyumbani hapa na kufululiza kulia kwa sababu ambayo hatukuielewa “ ni siku moja tu toka tuwafukuze mapaka hayo kwa mawe na aliyekuwa na hasira na paka hao zaidi alikuwa ni marehemu kwa kushirikiana na mwenzie mmoja walihakikisha mapaka hayo wanaondoka maha;li hapo kutokana na ada ambayo tulikuwa tunaipata.

Hivyo hadi habari hii inaindikwa, imedaiwa Joseph ameshindwa kutoka leo kwenda kwenye shughuli zake na hapa na pale kutoka na hali yake ya kiafya haijakaa sawasawa.

No comments:

Post a Comment