KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, August 3, 2010

Wanzanzibari wahalalisha mseto


ASILIMIA kubwa ya matokeo yaliyopigwa na wananchi kujibu ndiyo ama hapana kuridhia serikali ya mseto, serikali ya Umoja wa Kitaifa visiwani humo kura ya ndio ilishinda kwa vishindo kwa mujibu wa matokeo hayo.

Matokeo hayo yalitangazwa jana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Khatib Mwinyichande, baada ya kufanywa majumuisho kutoka ndani ya majimbo yote 50 ya uchaguzi visiwani Zanzibar.

Jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 293,039, na kura za ndio zilipatikana188,705 na hapana zilipatikana 95,613.

Hivyo kura za ndio zilikuwa asilimia 66

Kwa mujibu wa matokeo hayo Vyama vya CCM na CUF vimeunga mkono matokeo hayo ya kura ya maoni, ambapo Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alionekana kufurahia matokeo hayo ya kubadidlisha mfumo wa serikali kwa kusema mfumo huo utasaidia kumaliza matatizo ya kisiasa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment