KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, August 3, 2010

Mapozi ya Bwana na Bi Harusi Yamuua Mpiga Picha

Mpiga picha kwenye harusi nchini Sicily amefariki dunia kwa kupigwa risasi alipowapa bunduki bwana na bi harusi waweke pozi ili awapige picha ya ukumbusho.
Mpiga picha Calogero Scimea mwenye umri wa miaka 45 aliwapa bunduki bwana na bi harusi ili waweke pozi na bunduki hizo ili awapige picha ya ukumbusho.

Scimea alikuwa akipiga picha za harusi ya wapenzi wa tangia utotoni Valentina Anitra, 22, na Ignazio Licodia, 25, wakati alipowaambia watumie bunduki za kuwindia wanyama kuweka pozi.

Mojawapo ya risasi katika bunduki hizo ilifyatuka na kumuua mpiga picha mbele ya bwana na bi harusi pamoja na wazazi wao.

Ajali hiyo ilitokea muda mfupi kabla ya maharusi kwenda kanisani.

Taarifa zilisema mpiga picha huyo alifika kwenye harusi hiyo kuchukua nafasi ya rafiki yake ambaye alishindwa kufika kwenye harusi hiyo kutokana na ugonjwa.

Bunduki zilizotumika wakati wa tukio zilikuwa na vibali halali.

Polisi wanaendelea na uchunguzi.

No comments:

Post a Comment