KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, August 3, 2010

Kikwete atuma pole kwa Dk. Slaa

RAIS Jakaya Kikwete amemtumia salamu za pole kwa masikitiko, mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, kutokana na kuanguka kwake na kudaiwa amevunjika mkono.

Kikwete ametuma pole hizo na vilevile amemtakia Dk. Slaa apone kwa haraka ili kusukuma gurudumu vyema la mchakato wa uchaguzi unaoendelea hivi sasa

Salamu hizo zilisema “Nakuombea kwa Mwenyezi Mungu, akupe uwezo wa kupona haraka ili uweze kurejea katika shughuli zako za kutumikia umma wa watanzania.” alisema Kikwete

Mwishoni mwa wiki iliyopita siku ya Jumamosi majira ya usiku, akiwa mkoani Mwanza,Dk, Slaa alianguka akiwa bafuni na kusababisha apate maumivu makali yaliyosababishwa avunjike mkono na kukimbizwa hospitalini. .

Dk. Slaa alikuwa katika kampeni zake za kusaka ridhaa akip[ita kila mkoa nchini ikiwemo na kuomba wadhamini mikoani humo.

No comments:

Post a Comment