KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 31, 2010

Wanafunzi waweweseka Tabata


JANA katika Shule ya Msingi Tumaini iliyopo Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam, wanafunzi wake wa darasa la saba wameanguka na wengine kuzimia kwa kile kilichodaiwa ni mapepo iliyoikumbwa shule hiyo
Tukio hilo la aina yake, lilianza majira ya saa 2 asubuhi, katika chumba cha darasa la Saba’ B’ na wanafunzi hao kuanza kuanguka hovyo wakati mwalimu akiendelea kufundisha.

Ilidaiwa kuwa upepo mkali ulivuma na kupita ndani ya chumba hicho na baada ya dakika kadhaa wanafunzi hao wakaanza kuanguka na kupiga kelele .

Ilidaiwa na mwalimu aliyekuwa akifundisha wanafunzi hao somo la kiingereza darasani humo, MWalimu Wilbard alisema kuwa awali mwanafunzi Lightness alianza kudondoka na mwalimu huyo ali[poona hali alichukua maji aliyaombea na kumpa mwanafunzi huyo ayanywe na alikataa maji hayo punde mweanafunzi mmoja mmja alianza kuanguka na kupiga kelele kali.

Hata hivyo kutokana na kuzidi kwa hali hiyo kwa wanafunzi hao mwalimu mkuu wa shule hiyo, bi Anna Mang’enya liwaruhusu walimu wafanye kazi ya ziada kuanza kuwaombea wanafunzi hao lakini hali haikuweza kukaa sawa na kuanza kuwasilina na viongozi wa dini waje waombee wanafunzi hao wakiwemo mashekhe na mapadri.

Hivyo zoezi la kuombea wanafunzi hao lilidumu shuleni hapo kwa masaa kwa kadhaa.

Matukio ya aina hii hutokea mara kwa mara katika shule mbalimbali za msingi nchini hali

No comments:

Post a Comment