KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 31, 2010

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma yateketea


OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, imeteketea kwa moto jana na kusababisha nyaraka muhimu za serikali zilizokuwa katika ofisi hiyo kuteketea kwa moto
Moto ulizuka ghafla majira ya asubuhi, kwa chanzo ambacho hakikufahamika na kuteketeza nyaraka muhimu za serikali katika ofisi hiyo iliyokuwa na vyumba 35

Akielezea tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw. James Msekela alisema chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana na imesababisha serikali kuingia hasara kubwa.

Alisema moto huo ulianza kuwaka katiia moja ya chumba katika ofisi hizo na kuenea kote na kushindwa kuudhibiti hadi kusambaa jingo lote.

Hatya hivyo mkuu huyo aliulaumu uongozi wa zimamoto kwa kuchelewa eneo la tukio na kutowajibika kama ipasavyo.

Alisema ameunda timu maalum na kuwashirikisha watumishi ioli kubaini chanzo cha moto huo

No comments:

Post a Comment