KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 31, 2010

Chadema yawasilisha pingamizi


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana kimewasilisha pingamizi katika ofisi za Msajili wa vyama vya Siasa dhidi ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.


Pingamizi hilo liliwasilishwa jana, majira ya mchana na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama hicho Bw. John Mnyika.

Hiyo ni moja ya ahadi iliyotolewa na chama hicho kuwasilisha pingamizi hilo ambapo walidai kuwa kikwete alitengua sheria za uchaguzi wakati wa kuzindua kampeni za chama cha CCM.

Pingamizi hiyo inasema Kikwete azuiwe kugombea urais kwa kuwa chama hichokilisema Kikwete amekiuka Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa kutangaza nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi kwenye kampeni zake.

Vilevile Mnyika alisema Kikwete katika kukiuka kanuni hizo mgombea wa CCM, aliahidi kukilipia Chama cha Ushirika cha Nyanza deni la Shilingi bilioni 5 na kuahidi kununua meli kwa ajili ya watu wa mikoa ya Kagera na Mwanza hali ambayo ni amekwenda kinyume na kanuni za uchaguzi.

Mnyika alisema Kikwete alitumia cheo chake cha urais kutngaza ahadi kwenye kampeni hizo hali inayofanya kuwanunua wapiga kura kinguvu

No comments:

Post a Comment