KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, August 6, 2010

Wanafunzi 18 waangamia ziwa Victoria

Wanafunzi 18 wanahofiwa kuangamia katika ajali ya mtumbi katika ziwa Victoria nchini Tanzania.

Ajali hiyo ni ya tatu katika eneo hilo katika muda wa mwezi mmoja.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, boti hiyo ilikuwa imebeba abiria kupitia kisasi.

Mkuu wa wilaya ya Sengerema, David Palangyo amesema boti hiyo ilizama kutokana na hali mbaya ya anga.

Palangyo ameongezea kuwa boti hilo lilikuwa limebaba wanafunzi 37 waliokuwa na umri wa kati ya miaka 5 na 14.


Wavuvi ziwa Victoria
20 kati yao waliokolewa na maafisa wa polisi kwa ushirikiano na wavuvi katika ziwa hilo.

Duru zinasema mtumbwi huo ulikuwa ukielekea kisiwa cha Itendelea kutoka Lukungu.

Kamanda huyo wa polisi amesema uchunguzi umeanzishwa ili kubainisha chanzo cha ajali hiyo, lakini amekiri kuwa naodha wa mtumbwi huo amekamatwa na atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.


Siku ya jumapili wiki iliyopita mashua iliyokuwa na shehena na samaki na abiria ilizama katika eneo la ziwa hilo, inayomilikiwa na Uganda.

Watu 33 waliangamia kwenye ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment