KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, August 6, 2010

Afrika Kusini imemwita balozi wake Rwanda


Afrika Kusini imemwita nyumbani balozi wake nchini Rwanda, kufuatia mzozo wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili, kuhusu kujeruhiwa kwa aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Rwanda ambaye yuko mafichoni mjini Johanesburg.

Wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini imesema balozi huyo ameamrishwa kurejea nyumbani kwa mashauriano zaidi, lakini uamuzi huo haumaanishi kuwa Afrika Kusini imekatiza uhusiano wake na Rwanda.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje nchini Afrika Kusini, Ayanda Ntsaluba, amesema uamuzi huo hauna uhusiano wowote na tukio hilo la kujeruhiwa kwa mkuu huyo wa majeshi Faustin Kayumba Nyamwasa.

Generali muasi Faustin Kayumba Nyamwasa, alijeruhiwa kwa kupigwa risasi mwezi Juni mwaka huu mjini Johannesburg. Serikali ya Rwanda imekana kuhusika na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment