KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, August 6, 2010

Mpambe wa Mandela alipewa 'mawe ya Naomi'


Aliyekuwa mkuu wa mfuko wa kusaidia watoto wa Nelson Mandela, Jeremy Ratcliffe, alisema alipokea almasi ambazo hazikuchongwa kutoka kwa mwanamitindo Naomi Campbell.

Alitoa kauli hiyo baada ya Bi Campbell kutoa ushahidi wake kwenye kesi ya uhalifu wa kivita inayomkabili kiongozi wa zamani wa Liberia Charles Taylor.

Inadaiwa alipokea almasi hizo kutoka kwa Bw Taylor mwaka 1997, zinazoweza kumhusisha na 'almasi haramu zinazotumika kugharamia vita'

Bw Ratcliffe alisema yuko tayari kutoa ushahidi The Hague na kwa sasa amekabidhi mawe hayo kwa mamlaka husika.

Alisema katika taarifa iliyopelekwa BBC, " Nilipewa almasi tatu ndogo ambazo hazikukatwa na Naomi Campbell tarehe 26 Septemba, 1997."

Katika kesi hiyo, Bi Campbell alisema alipewa "mawe machafu" baada ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela ambapo Bw Taylor naye alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa.

Alisema watu wawili ambao hawakuwafahamu walikwenda chumbani kwake na kumpa mawe hayo.

Aliiambia mahakama kuwa hakuwa na ushahidi wowote kuwa zilitoka kwa Bw Taylor na alimpa Bw Ratcliffe kwasababu alitaka mawe hayo yatolewe kwenye mashirika ya hisani.

No comments:

Post a Comment